Doreen Aloyce, Unguja.
IMEELEZWA kuwa nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na changamoto ya kukauka kwa maji ikiwemo Zanzibar jambo ambalo limepelekea wadau wa ngazi za juu wa ushirikiano Katika uwekezaji wa Sekta ya maji kusini mwa Aftika (GWPSA) kuweka mkakati wa pamoja kuona namna ya kukabiliana na tatizo hilo.
Hayo yalibainishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ,Dkt Hussein Mwinyi wakati alipokuwa kwenye ufunguzi wa mkutano wa wadau hao uliofanyika Hotel ya Kiwengwa Melia Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Aidha Dkt Mwingi anasema mkutano huo umekuja wakati muwafaka ambapo kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa sehemu nyingi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini kumekua na changamoto kubwa ya upungufu wa maji.
"Hapa Zanzibar nimekuwa nikipokea taarifa za kuendelea kukauka visima mbalimbali vinavyotumiwa na wananchi,"alisema.
Anasema ili kutekeleza mipango ya maendeleo kwa ufanisi katika sekta ya viwanda, utalii, ujenzi, miundombinu na kutoa huduma bora za afya na elimu ni lazima kuwa na huduma ya maji safi na salama ya uhakika.
Rais Mwinyi anabainisha kwamba ni matumaini yake mapendekezo ya maazimio yatakayopitishwa katika mkutano huo yatakuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha malengo ya kuazishwa programu hiyo pamoja na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizopo katika sekta ya maji.
Anasema Febuari, 2021 Umoja wa Afrika ulipitisha programu za uwekezaji katika sekta ya maji barani Afrika kwa lengo la kuimarisha uwekezaji na usalama wa maji safi na mazingira barani humo
Kuwa viongozi wa ngazi ya juu wa nchi washirika wameanzisha fomu ya tathmini ya utekelezaji wa programu hiyo hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuunga mkono uamuzi huo kwani fomu hiyo itahamasisha uwekezaji wa pamoja na kuimarisha uwekezaji baina ya sekta za umma na sekta binafsi.
Amesema mkutano huo kwake ni muhimu kwani amekuwa akijiuliza mbinu bora za kufanya ili kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama Zanzibar ambayo bado inawakumba wananchi katika maeneo mbalimbali ya visiwa vya Unguja na Pemba.
“Leo nimefurahi sana kushiriki katika mkutano huu ambao naamini utatoa uzoefu kwa wataalamu wetu mbalimbali walioshiriki katika kongamano hili ili nasi tuweze kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wetu,” amesema.
Hivyo ni matarajio yake kwamba mkutano huo utaweza kuonesha fursa za uwekezaji zilizokuwepo katika sekta mbalimbali za uchumi huo ikiwemo utalii, uvuvi, bandari, usafiri wa baharini na mafura na gesi.
Naye Mwenyekiti wa GWPSA, Jakaya Kikwete anasema wapo watu wanaokabiliwa na changamoto ya maji barani Afrika inayosababishwa na mabadililo ya tabia ya nchi.
Kikwete ambaye pia ni Rais mstaafu awamu ya Nne wa Tanzania anasema ili kuondokana na tatizo hilo ni lazima miradi mikubwa ya maji itekelezwe kwa haraka ili kukabiliana na changamoto hiyo katika nchi za Afrika.
Anasema wana programu ambayo imepitishwa katika mkutano wa 34 wa Afrika na upo mfumo uliotengenezwa ili kufikia malengo ya uanzishwaji wa programu ya maji Afrika.
Kikwete anasesema uwekezaji wa maji unaohitajika barani Afrika gharama zake ni dola bilioni 64.
Anaelezaa lazima viongozi wa nchi za Afrika wawe na mkakati wa pamoja kutoa kipaumbele kuongeza kasi ya upatikanaji wa maji katika mataifa yao.
"Nchi za Afrika lazima ziweke mazingira mazuri ya uwekezaji ili kuvutia sekta binafsi kuwekeza zaidi kwenye maji jambo litakalosaidia kuondoa adha ya huduma hii muhimu kwa ustawi wa wananchi," alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Umoja wa Maendeleo Afrika, Ibrahim Mayaki akizungumza kwa njia ya mtandao, anasema kuna mahitaji makubwa ya kuleta mabadiliko katika nchi za Afrika na Umoja wa mataifa katika sekta hiyo muhimu.
Kwa upande wao wananchi wakizungumza na majira Gazeti wanasema kuwa maeneo mengi wanayoishi Kuna shida ya maji na mengine ni ya chumvo na magadi hivyo kupitia majadiliano hayo yataenda kuleta tija kubwa kwao na Taifa kwa ujumla.

